24 September 2014

Jay Z ashitakiwa kwa kuimba kionjo cha wimbo 'Run This Town', naye ajibu tuhuma

Rapper Jay Z anakabiliwa na kesi akituhumiwa kusample bila kibali kionjo cha wimbo wa mwaka 1969 na kukitumia kwenye wimbo wake Run This Town wa mwaka 2009.
Record label ya TufAmerica imetangaza kuwa inamshitaki Jay Z kwa kusampe ‘Oh’, sio sentensi wala neno, ile “Oh” inayosikika kwenye Run Town. Record label hiyo inadai aliisample bila ruhusa kutoka kwenye wimbo Eddie Bo wa mwaka 1969 ‘Hook and Sling’.

Hata hivyo, Jay Z aliamua kujibu kupitia mwanasheria wake ambaye alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa hakukuwa na mantiki ya kiubora wala kiukubwa kuwa alisampo syllable hiyo.
“Even if one short word – or the recording thereof – could possibly be deemed original enough to warrant copyright protection, this fleeting and generic phrase is neither quantitatively nor qualitatively significant.”

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname