26 September 2014

"Hata iweje siwezi kuachana na Nuh Mziwanda" - Shilole huyo

 
Baada ya varangati lililotokea Tabora katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,  baada mpenzi wa mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,  Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kukataliwa na mashabiki, Shilole ameamua kufunguka kuwa Nuh atabaki kuwa mpenzi wake katika hali yoyote.
Akizungumza na paparazi wa kampuni ya GPL, Shilole alisema lengo lake lilikuwa ni
kumtambulisha mpenzi wake kwa mashabiki wake japo walimkataa kuwa shemeji yao.
“Wakati namtambulisha Nuh kwa wakazi wa Tabora kuwa shemeji yao kiukweli nilishindwa kuelewa kwa nini nilizomewa ila ninachoweza kusema tena wakubali, wakatae Nuh atabaki kuwa shemeji yao tu,” alisema Shilole.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname