NYOTA
wa kuigiza sauti za watu maarufu aliye pia mwigizaji wa sinema za
Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wikiendi iliyopita alijikuta
akiaibika kwa kuzomewa na kupopolewa kwa chupa za maji na mashabiki
wa Klabu ya Simba baada ya kuingia uwanjani na demu aliyevaa
‘kihasarahasara’.Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’akiwa na mrembo huyo.Ishu hiyo ilijiri Jumamosi ya Septemba 20,
2014 ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini hapa wakati wa pambano kati ya
Yanga na Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wenyeji
walishinda 2-0.
Steve alitinga uwanjani saa 11:00 jioni akiwa na demu huyo mrefu kwake,aliyetinga kipensi cha jinzi kifupi na tisheti ya njano na kijani (zinazotumiwa na Yanga).
Steve alitinga uwanjani saa 11:00 jioni akiwa na demu huyo mrefu kwake,aliyetinga kipensi cha jinzi kifupi na tisheti ya njano na kijani (zinazotumiwa na Yanga).
Wakati wawili hao wakipita kwenye jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo walipozomewa
na wengine kuwarushia chupa za maji kwa kile kilichodaiwa kuwa, demu
huyo alivunja maadili ya Kitanzania kwa kuvaa kihasara hadharani
No comments:
Post a Comment