Kwa mara nyingine tena, mashabiki wa Diamond Platnumz wameshindwa kumuona akitumbuiza licha ya kumsubiria hadi saa 10 Alfajiri.Awamu hii imetokea jijini London, Uingereza katika show aliyoitangaza kwa kiasi kikubwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Tofauti na Stuttgurt, Ujerumani ambako mashabiki walifanya uharibifu mkubwa, mashabiki wa London waliamua kuwa wapole tu na kurejea majumbani mwao na hasira walizozimeza vifuani.
No comments:
Post a Comment