16 August 2014

TRAFIKI WAMFUNGIA KAZI DEREVA JEURI DAR!

  Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimdhibiti dereva wa basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) aliyevunja sheria ya usalama barabarani.
 DEREVA wa Basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, amejikuta akipewa kibano hevi na askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ baada ya kuleta ubabe wakati alipotakiwa kutii sheria bila shuruti.Tukio hilo la aina yake lililosababisha usumbufu kwa abiria wa basi hilo, lilitokea juzi Bamaga-Mwenge jijini Dar kufuatia dereva huyo kukataa kuegesha pembeni basi hilo lenye namba za usajili T 619 CVP lililokuwa limevunja sheria ya usalama barabarani.



Dereva huyo akionyesha ubishi wa kutotii maagizo ya 'trafiki'.
Imedaiwa kuwa, basi hilo lilishusha abiria kinyume na sheria kwenye kituo kisicho rasmi maeneo ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Barabara ya Shekilango.PICHA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname