10 August 2014

RPC NJOMBE APATA AJALI NA MLINZI WAKE AFARIKI DUNIA

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ASP Fulgence Ngonyani.
Na James Festo, Njombe.
KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  pamoja na dereva wake Nuaka Seme  wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Njombe ya kibena ambako wanaendelea  kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia  jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia papo hapo.



Akiongea na vyombo vya habari  huku akipatiwa matibabu katika hospitari ya Mkoa kutokana na Mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe ASP Yahaya  rajab kushindwa kuongea kwa madai kuwa hanaruhusa Kamanda Ngonyani alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu hadi saa nne za usiku katika barabara ya  Makambako hadi Njombe.PICHA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname