Mwanadada mwigizaji na mwanamuziki Zuwena Mohamed 'Shilole' akicheza kwa kujiachia katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 usiku wa kuamkia leo.
Roma
Mkatoliki akiwarusha vilivyo wapenzi wa burudani waliofurika katika
Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 usiku wa kuamkia leo.
Roma Mkatoliki akiongea na mashabiki wake.
Mashabiki wakiendelea kucheza na Roma.
Roma Mkatoliki akiendelea kufanya makamuzi.
Staa
kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha
la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Staa
kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade akipiga shoo katika Tamasha la Usiku
wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Makamu
wa Rais Mh. Mohamed Gharib Bilali akisalimiana Makamu wa rais
Mh.Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na Miongoni mwa matukio
yaliyosisimua kwenye tamasha hilo ni pale mechi za mpira wa miguu
zilipokuwa zikichukua nafasi.
Yemi Alade akipiga shoo.
BONGO MOVIES VS BONGO FLEVAWakati mechi hiyo ilipokuwa ikikaribia kuanza, umati ulilipuka kwa shangwe baada ya kumuona Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba alipokuwa alipoonekana akipasha misuli na wenzake.
Mwanamuziki H-Baba akijaribu kuwatoka wachezaji wa Bongo Movies.
Wengi
walikuwa wakishangilia wakidai ni siku nyingi hawajamuoana uwanjani,
huku wengine wakishangilia kwa kuimba wimbo wake mpya wa Mwana.
Mchezaji wa Bongo Fleva, Ali Kiba akimtoka msanii wa Bongo Movies, Issa Mussa 'Cloud 112'.
Kama
hiyo haitoshi haitoshi, shangwe zaidi liliongezeka baada ya Kiba
kufunga bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya Bongo
Fleva waibuke kidedea kwa mara nyingine hivi kumfanya kuwa nyota kwenye
tamasha hilo.
Nyomi iliyokusanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar kwa ajili ya Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
BONGO MOVIES WACHEZA KIDUKULicha ya kufungwa, mashabiki wa Bongo Movies ndiyo walionesha kushangilia zaidi ya mashabiki wa Bongo Fleva ambao ndiyo walikuwa washindi.
Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
Walicheza staili ya kiduku ile mbaya huku wakishangiliwa na umati uliofurika uwanjani hapo.
Bondia
Mada Maugo amemshushia kichapo bondia Thomas Mashali katika mpambano
wao kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa
jijini Dar.
WABUNGE SIMBA VS YANGAWakati wa mechi ya wabunge, vituko ndiyo ilikuwa balaa. Kuna wakati baadhi ya waheshimiwa wabunge walikuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kusogea lakini mwisho wa siku ilikuwa ni burudani kwani waliweza kubadilishana, wengine wakachukua nafasi. Hadi mtanange unamalizika, wabunge wa Yanga waliibuka kidededea kwa ushindi wa mabao 3 kwa 2.
Yanga wakishangilia bao lao.
Matukio
mengine yaliyosisimua siku hiyo ni kama wasanii wa Bongo Fleva, Juma
Nature, Shilole na wengineo ambao walipanda stejini kwa nyakati tofauti
na kutoa burudani baab’kubwa.Tamasha la Usiku wa Matumaini mwaka huu lilikuwa noma sana!
Ridhiwan Kikwete akishangilia ushindi wa Yanga dhidi ya Simba.
No comments:
Post a Comment