Rolf alikuwa amejipanga kufanya onesho la sarakasi na kikundi chake nchini humo ambapo huonesha michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘kumeza mapanga’.
Ameieleza Association Press kuwa maafisa wa uhamiaji walikuwa tayari wameshaweka stamp kwenye Passport yake na kumruhusu kuingia lakini alizuiwa baadae kabla hajavuka eneo hilo.
Club aliyokuwa amepanga kufanyia onesho hilo imeeleza kuwa, ilitumiwa barua pepe inayoeleza kuwa uongozi wa Uwanja wa ndege ulitaja ‘sababu za usalama’ kuwa chanzo cha katazo hilo.
Rolf Buchholz anatajwa kuwa mtu mwenye tattoo nyingi zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment