Baadhi ya wafanyakazi wa Global, wakifuatilia kwa makini hafla hiyo.
Eric Shigongo akimlisha keki Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.
Mmoja ya wakurugenzi wa Global, Lydia Bukumbi akimlisha keki Erick Shigongo.
Eric Shigongo akimlisha keki Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota.
Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally akilishwa keki.
Eric Shigongo akimlisha keki Mhariri msadizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli.
Mhasibu Sakina Yusufu akilishwa keki na Eric Shigongo.
Mwandishi Wilbert Molandi akijiandaa kulishwa keki.
Baadhi ya wafanyakazi wa Global wakiendelea na shangwe za 'bethidei' ya Shigongo.
Shigongo akifungua Shampeni.
Wafanyakazi wakiwa wameelekeza nadhari kwa mkurugenzi wao wakati akitoa nasaha zake.
Na Gladness Mallya WAFANYAKAZI wa
kampuni ya Global Publishers Ltd inayochapisha magazeti ya Ijumaa
Wikienda, Uwazi,Risasi, Amani, Ijumaa na Championi leo asubuhi
walimfanyia sapraiz ya bethdei Mkurugenzi Mtendaji wao, Eric Shigongo,
ambaye alitimiza miaka 46.Tukio hilo la aina yake lilifanyika juzi Jumatatu asubuhi ambapo taa zilizimwa ofisi nzima na Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally akamfuata ofisini kwake akimuomba aje kwenye chumba cha habari.
Ilikuwa ni shangwe pale alipotoka kwani taa ziliwashwa huku wafanyakazi wakiimba na kumshangilia wakati yeye akibaki ameduwaa kwani lilikuwa ni tukio la ghafla ambalo huenda alikuwa tayari amelisahau.
Baada ya hapo alikabidhiwa shampeni na kabla hajaifungua aliwashukuru wafanyakazi kwa kumfanyia sapraiz hiyo kwani alikuwa hakumbuki kama ni siku yake ya kuzaliwa.
Katika maneno yake ya shukurani kwa wafanyakazi, Shigongo ambaye alionekana mchangamfu na mwenye afya njema, kama ilivyokawaida yake, aliwaomba kudumisha upendo miongoni mwao kama familia na kwa kusaidiana katika kuimarishana kikazi.
“Nawashukuru sana jamani na namshukuru Mungu kwani nimekua sasa na leo nimetimiza miaka 46, siyo kitu rahisi ila ni mkono wa Mungu ulionifikisha hapo. Nawaomba tuendelee kufanya kazi kwa bidii na kwa umoja tulionao,” alisema.
Baada ya zoezi la kufungua shampeni, lilifuata zoezi la kukata keki ambapo ‘mzaliwa’ aliwalisha wafanyakazi wengi kabla ya kupata nao kifungua kinywa (chai).
No comments:
Post a Comment