Mwimbaji
wa kike aliyepiga hatua kubwa hivi karibuni na kusainiwa na kampuni ya
kubwa ya Afrika Kusini NFZ, Linah alifanya mahojiano exclusively na
tovuti ya Times Fm na kufunguka zaidi kuhusu mambo muhimu katika muziki
wake.Linah
alizungumzia masuala muhimu yanayohusu muziki wake. Jinsi alivyofanya
kazi na kundi la Uhuru ‘Ole Themba’ na alivyojipanga kulikabili soko la
kimataifa.
Mwimbaji
huyo alieleza pia mtazamo wake kwa ushirikiano kati ya wasanii wa kike
na sababu inayowafanya kutokuwa pamoja na kusapotiana pamoja na mambo
mengine.
Ameeleza
pia kama ana mpango wa kwenda Big Brother na mtu anaempendekeza zaidi
kwenda katika jumba hilo, na kuweka wazi reaction yake baada ya kupata
taarifa kuwa aliyewahi kuwa mpenzi wake Amini amefunga ndoa
kimyakimya.Isikilize hapa utapata taarifa kiundani kuhusu yote
anayoyazungumza.
No comments:
Post a Comment