Kijana aliyekatwa na sime kichwani.
Timbwili lenye ujazo mkubwa limeibuka baa ambapo jamaa mmoja muokota chupa za maji ambaye jina lake halikupatikana, anadaiwa kukatwa sime kichwani na mwenye gari baada ya kukutwa amekaa karibu na gari hilo.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo la kuumiza lilijiri wikiendi iliyopita mishale ya asubuhi kwenye baa mpya iitwayo Kangaroo iliyopo eneo la Afrika Sana jijini Dar.Ilielezwa kwamba kijana huyo alikuwa amekaa pembeni ya gari hilo huku akisoma Gazeti Pendwa la Amani ambalo ni ndugu na hili, mara ghafla alikuja mtu akitokea ndani ya baa kisha akaingia kwenye gari lake aina ya Toyota Noah akatoka na sime na kuanza kumshambulia jamaa huyo kichwani.
Aliyemkata mwenzie na sime (kushoto) maeneo ya baa mpya iitwayo Kangaroo iliyopo eneo la Afrika Sana jijini Dar es Salaam.
Kufuatia tukio hilo, watu walijaa na kufunga mtaa wakishangaa kilichotokea huku aliyefanya kitendo hicho akikimbilia ndani ya baa kujinusuru na raia wenye hasira kali waliotaka kumlipizia kwa kumuua baada ya kugundua kuwa kijana huyo aliyeshambuliwa hakuwa mwizi.SOMA ZAIDI >>
No comments:
Post a Comment