Makamu wa Simba Kaburu akiwatambulisha Kisiga na Maguri leo |
Klabu
ya Simba leo imewatambuliasha wake wawili kingo Shabani Kisinga na
mshambuliaji Elias Maguri kwa ajili ya kuimarissha kikosi chao kuelekea
kwenye msimu mpya wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Wachezaji
hao wametambulishwa makao makuu ya klabu hiyo na makamu wa Rais wa
klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu ambaye amesema zoezi la usajili kwa
klabu yao bado linaendelea.
Kisiga
anajiunga na wekundu hao kwa mara ya pili mara baada ya kumaliza
mkataba wake na wakata miwa wa Mtibwa Sugar ambao alikuwa nao kwa miaka
miwili na sasa akijiunga na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kwa Upande wake Maguri ambaye alikuwa akiichezea Ruvu shooting ya Pwani ameingia kandarasi ya miaka miwili.
No comments:
Post a Comment