Kama sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website, blogs, facebook, twitter na Instagram inawezekana hii stori ya Gwajima ambae ni Muhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara moja.Hata hivyo Muhubiri mwenzake Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014 amenukuliwa na gazeti la Nyakati na kuizungumzia hiyo Helikopta akisema ‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili kinastahili kufurahiwa na Wakristo wote wa kweli, tujifunze kupongezana.. nampongeza sana’
‘Kumiliki kwake Helikopta kutachangia katika kufuta dhana potofu ambayo imedumu kwa muda mrefu ya kuyaita Makanisa ya kilokole…. makanisa ya vichochoroni, Helikopta sio starehe na hata muundo wake sio wa starehe bali ni kazi, itamwezesha pia kufika maeneo ambayo gari sio rahisi kumfikisha kutoa neno la Mungu’ – KakobeSOMA ZAIDI>>
No comments:
Post a Comment