12 August 2014

Audio: Diamond awashauri wanaotaka kushindana nae Tanzania



Joto la ushindani kati ya wasanii wa Tanzania linazidi kupanda huku mashabiki na vyombo vya habari wakidaiwa kuchochea kuni kwa namna moja au nyingine.
Diamond Platinumz ambaye ndiye msanii anaekabiriwa na ushindani mkubwa zaidi kwa sasa kwa kuwa yuko mstari wa mbele zaidi wa mafanikio katika muziki hapa nchini na kuvuka mipaka kuiwakilisha Tanzania, amewashauri wasanii wanaotaka kushindana nae kutojikita katika ushindani wa nyumbani.

Diamond alifunguka katika mahojiano aliyofanya na The Jump Off ya 100.5 Times Fm na Jabir Saleh kabla hajapokea tuzo ya AFRIMMA kama mwimbaji bora wa kiume Afrika Mashariki.
“Tutanue mawazo, tuache mawazo ya kushindana wenyewe kwa wenyewe Tanzania. Labda kuleta mabadiliko yataleta mabadiliko ya Chalinze, mababadiliko ya Dar es Salaam au wapi. ‘Tukakomeshana tukikutana kwenye show labda ya Mwembe Yanga,’ tuache hizo fikra.” Alisema Diamond.
“Kwa sababu sisi tunaweza tukafikiri hapa kuna pesa nyingi sana lakini hakuna pesa nyingi kama ukifirikia kule mbele. Kwa sababu mbele unaweza kupiga show mpaka dola 100,000 ambayo ni kama milioni 160 au 170. And that’s the only way we can make a lot of money.
“Nafikiria huu ni wakati wetu sisi, tufocus sasa na mbele kuliko kufocus hapa tunakuwa tunabishana sehemu ambayo ni padogo. Hapa tu kwenye chumba kimoja tunang’ang’ania humuhumu, huyu kashika mlango hatoki…wakati huku kuna sebule kuna nini…” Aliongeza.
Mkali huyo wa MdogoMdogo ameeleza kuwa wakati akiwa katika tuzo za BET alikuwa anaona jinsi ambavyo baadhi ya watu walivyotengeneza makundi na kuanza kumdiss bila sababu. Lakini yeye kwake hiyo huwa inampa nguvu zaidi ya kuwaza kuwa ni muda wa kuwakomesha kwa kutoa vitu vikali zaidi.
Msikilize hapa:

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname