06 July 2014
Xclusive: Nahreel apata shavu la kufanya kazi na label ya Choclate City ya Nigeria, wamtafuta baada ya kusikia beat zake
Producer ambaye ameshafanya hits nyingi hapa nyumbani zikiwemo ‘Come Over’ ya Vanessa Mdee na single mpya ya Mwana FA ‘Mfalme’, Nahreel ametafutwa na label kubwa ya Nigeria inayomsimamia muimbaji wa Kenya Victoria KImani baada ya kuwakuna kwa beat zake zenye vionjo vingi vya Kiafrika.
Nahreel ambaye kwa sasa anafanya kazi kwenye studio ya msanii Quick Racka ‘Switch’, amesema Choclate City walimtafuta wenyewe baada ya kusikiliza beat alizompa Victoria Kimani alipokuja Tanzania.
“Hivi juzi tu nimetafutwa na Choclate City kutokana na beat nilizompatia Victoria Kimani kipindi flani, kwahiyo juzi wameni approach walikuwa wanataka niwatumie beat nyingi ili waweze kufanya wasanii ambao wako chini ya label ya Choclate City”.
Ameendelea,
“Mpaka hivi sasa tuko kwenye mazungumzo na tayari beat nyingi nimeshawatumia, hawajaniambia ni nani na nani watakaohusika kuzitumia hizo beat kwahiyo hizo updates watanipa soon, lakini wamezikubali.”
Upande wa kundi lake na mpenzi wake Aika, Navy Kenzo pia wanamipango ya kuanza kushirikiana na wasanii wa kimataifa.
“Navy Kenzo pia tunatarajia kufanya collabo na wasanii wakubwa kutoka Nigeria, South Afrika kama Olamide, Manifesto wa Ghana ni watu ambao tuko kwenye mawasiliano nao na tunatarajia kufanya nao collabo hivi karibuni”.
“Mpaka mwisho wa mwaka huu tutakuwa tumefanya track nyingi sana ambazo tutakuwa tumeshirikisha watu, kwasababu watu wamekuwa wakitu-judge kwanini hamfanyi collabo na watu flani na nini ni Navy Kenzo tu, kwahiyo sasa hivi tuko katika hiyo mipango”. Alimaliza Nahreel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment