15 July 2014

WAMETISHA SANA: KIKOSI CHA ARSENAL MSIMU HUU NI SHIDAAAAA...JIONEE MWENYEWE HAPA...

ARSENAL imechoka kuburuzwa na sasa msimu ujao kwenye Ligi Kuu England moto utawaka.

Alhamisi iliyopita ilimnasa Alexis Sanchez kutoka Barcelona kwa uhamisho wa Pauni 30 milioni na kuwa mchezaji ghali wa pili kwenye klabu hiyo baada ya Mesut Ozil aliyesajiliwa mwaka jana kutoka Real Madrid.
Kocha Arsene Wenger amewavuta Sanchez na Mathieu Debuchy kwenye kikosi chake huku akipiga hesabu za kumnasa Morgan Schneiderlin sambamba na Sami Khedira.

Ujio wa mastaa hao wapya wataifanya Arsenal kuwa na kikosi matata msimu ujao, huku kiungo Mwingereza Jack Wilshere akidaiwa kuwa hana nafasi ya kupenya kikosini.

Wakati kikosi hicho kikiwa hakisajili straika yeyote wa kati hadi sasa, Olivier Giroud bado ataendelea kutesa kwenye namba yake, lakini Wenger msimu ujao atakuja kivingine ambapo Giroud atakuwa mbele ya mastaa watatu hatari, Theo Walcott, Ozil na Sanchez.

Schneiderlin na Aaron Ramsey watasimama kwenye sehemu ya kiungo na kuwafanya watu kama Mike Arteta, Santi Cazorla, Tomas Rosicky kuanzia benchi.  

Wenger amepanga kumaliza ukame wa mataji kwenye klabu hiyo kwa kuhakikisha anakuwa na kikosi imara kuanzia wanaoanzishwa hadi wachezaji wa benchi. Aliyepo uwanjani matata, anasubiri benchi ni hatari.


Anachosubiri Wenger ni kumnasa ama Schneiderlin kutoka Southampton ili kufunga hesabu zake na haitakuwa tatizo kama atashindwa kumpata Khedira kutoka Real Madrid.  

Kwenye benchi la Arsenal kutakuwa na wakali wengine hatari, Alex Oxlade-Chamberlain, Lukas Podolski, Nacho Monreal na Mathieu Flamini.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname