Mshike mshike wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Real Madrid
dhidi ya AS Roma, uliingia katika mzimu wa mpambano wa mahasimu wakubwa
nchini Hispania baada ya beki kutoka nchini Ureno Pepe kukwaruzana na
kiungo kutoka nchini Mali, Seydou Keita.
Wawili hao walikwaruzana kabla ya mpambano huo wa kujiandaa na msimu
haujachezwa katika mji Dallas, nchini Marekani ambapo Pepe alionekana
akirushiwa chupa ya maji hali ambayo ilizua tafrani kabla ya kuamuliwa
na wachezaji wenzao.
Pamoja na madhila yoye hayo Pepe alionekana ni mwenye kutabasamu na kuyapuuza yaliyotokea.
Hata hivyo kitendo hicho kilipelekea hasira kwa Keita na kujikuta
akifanya maamuzi ya kutompa mkono Pepe wakati wachezaji wa AS Roma
walipokuwa wakiwasalimu wachezaji wa Real Madrid kabla ya mchezo huo wa
kirafiki kuanza.
Hii si mara ya kwanza kwa wachezaji hao kukwaruzana, kwani kama
itakumbukwa vyema wakati wa mchezo wa Spanish Supercopa wa mwaka 2011
kati ya FC Barcelona dhidi ya Real Madrid, Keita alilumbana na Pepe
baada ya kuchikizwa na maneno ya kibaguzi ambayo alidai alitamkiwa na
beki huyo kutoka nchini Ureno
Mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya AS Roma ulichezwa usiku wa kuamkia jana, ambapo mabingwa wa barani Ulaya The Meringues walikubalia kulala bao moja kwa sifuri.
No comments:
Post a Comment