UHOLANZI
imeonesha ubora wake kwa kuipiga Brazil mabao 3-0 jana usiku na kutwaa
nafasi ya tatu ya kombe la dunia, kwa mujibu wa kocha Louis van Gaal.
The
Orange ilipata ushindi mnono dhidi ya wenyeji na shukurani kwa mabao ya
Robin Van Persie, Daley Blind na Georginio Wijnaldum, ambapo ilikuwa
mechi ya mwisho kwa Van Gaal kuiongozo Uholanzi kabla ya kuanza kazi
mpya katika klabu ya Manchester United.
Kocha
huyo alisema alikuwa na furaha kuona wachezaji wake wameimarika vizuri
kufuatia kufungwa na Argentina katika mchezo wa nusu fainali.
“Ilikuwa ngumu sana kwetu,” Van Gaal aliwaambia NOS baada ya mchezo. “Ugumu wote ulikuwa kwetu. Brazil walikuwa angalau na siku zaidi ya maandalizi na tulifungwa kwa penati”.
“Tungekuwa
fainali. Morali yetu ilishuka baada kufungwa na Argentina.
Nitazungumzia mechi ya Brazil katika mazungumzo na timu yangu na sio
kuhusu Argentina. Kwa bahati nzuri tumeonesha tena jinsi gani tuna
ubora”.
Kipa
wa Swansea, Michel Vorm aliingia katika dakika ya mwisho , inamaanisha
Uholanzi imewatumia wachezaji wote 23 katika fainali za 2014 nchini
Brazil.
No comments:
Post a Comment