14 July 2014

UJERUMANI YASHINDA UBINGWA WA DUNIA...NA HAWA NDO WACHEZAJI WALIO SHINDA TUZO MBALIMBALI




Baada ya takribani siku 30 hatimaye michuano ya kombe la dunia imemalizika.

Mchezo wa fainali uliwakutanisha Ujerumani dhidi ya Argentina – mechi ikipigwa jijini Rio De Jeneiro kwenye uwanja wa Maracana.

Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa 1-0 kwa Ujerumani.


Goli pekee la dakika 30 za nyongeza la Mario Gotze likaipa Ujerumani ubingwa wake wa nne wa dunia.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu kutoka Ulaya kutwaa ubingwa wa dunia ndaninya ardhi ya Amerika.

Wakati huo huo tuzo ya mchezaji bora wa mashindano imeenda kwa Lionel Messi, mfungaji bora James Rodriguez, kipa bora Manuel Neur na mwanasoka bora chipukizi wa mashindano amechukua Paul Pogba.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname