Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akiingia kwenye
ukumbi wa mkutano wa Town Hall ambao baadaye yeye na viongozi vijana
wenzie watakutana na Rais Barak Obama wa Marekani atakapozungumza nao
jijini Washington DC.
Hii ni sehemu ya
program ya mafunzo kwa viongozi wadogo walioonyesha dira toka nchi zote
za Afrika (most promising young African leaders) . Program hii
imeanzishwa na Rais Obama mwenyewe.
Miongoni mwa
watanzania wachache waliopata fursa ya kuhudhuria ni Naibu Waziri wa
Nishati na Madini Mhe. Steven Masele na Mhe. Joshua Nassari. Watakutana
pia na Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry na Mke wa Rais
Obama Bi Michelle Obama Pamoja na maseneta, Magavana, wafanyabiashara
wakubwa an watu wengine mashuhuri
No comments:
Post a Comment