ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.
Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha
viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli
zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo
vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bacteria au fangasi wanaoleta
magonjwa. Kwa
kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia
huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi
na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin (Bartholin's glands) zilizopo
kwenye shingo ya mlango wa uzazi (Cervix).
Sababu za kutokwa na uchafu huo Kuna sababu nyingi ambazo husababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya kawaida kutoka kwenye sehemu zake za siri. Maambukizi ya bacteria wanaosababisha magonjwa kama Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorhear au uambukizo wa bacteria Candida albicans, Vaginosis Bacteria n.k husababisha mwanamke kutokwa na uchafu
unaoambatana na harufu mbaya.
Pia mabaki ya vitambaa, tissue au pedi ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi huweza kusababisha tatizo hili. Usafi wa sehemu za siri usipozingatiwa hususani mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, huweza kuwa mazalia mazuri ya bacteria wanaosababisha harufu mbaya.
Dalili za ugonjwa wa kutoa harufu Wanawake wenye tatizo la Vaginosis huwa na dalili kubwa ya kutokwa na ute na majimaji yasiyo ya kawaida (Uchafu) kutoka sehemu za siri. Uchafu huu huwa unatoa harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu. Wakati mwingine uchafu wenye rangi kama ya kijani
hutoka -Kuwashwa na kuchomachoma sehemu za siri, mgonjwa asipopatiwa tiba haraka husababisha vidonda sehemu za siri.
- Mwanamke anapoona anatokwa na ute uliochanganyikana na damu hata kama hayupo kwenye siku zake, hii ni dalili nyingine ya Vaginosis. - Maumivu makali wakati wa tendo pia ni dalili za ugonjwa huu.
Tatizo
hili hutibika hospitalini baada ya vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na
daktari au nesi mwenye uzoefu wa kutosha juu ya magonjwa ya wanawake.
Dawa za kupaka (Ointment/ Cream) na dawa za kumeza (Pills) huweza
kumaliza tatizo hili.
Kumbuka: Ni makosa kutumia
dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari au nesi.
Jihadhari
wanawake wengi hupenda kutumia baadhi ya dawa ukeni kwa lengo la kuongeza vionjo kwenye mapenzi pia kuufanya uke kunukia vizuri vitu hivyo ni kama sabuni za kukaza uke, shabo inayowekwa kwenye maji machafu ili kusafisha wenyewe huweka ukeni ili kukaza uke, dawa za kusafishia ukeni hasa zenye kemikali, hudi asali na vingine vingi naomba niseme kuwa njia hizi hufurahisha kwa mda mfupi lakini madhara yake ni makubwa kama hivyo
kuanza kutoa harufu mbaya.
wanawake wengi hupenda kutumia baadhi ya dawa ukeni kwa lengo la kuongeza vionjo kwenye mapenzi pia kuufanya uke kunukia vizuri vitu hivyo ni kama sabuni za kukaza uke, shabo inayowekwa kwenye maji machafu ili kusafisha wenyewe huweka ukeni ili kukaza uke, dawa za kusafishia ukeni hasa zenye kemikali, hudi asali na vingine vingi naomba niseme kuwa njia hizi hufurahisha kwa mda mfupi lakini madhara yake ni makubwa kama hivyo
kuanza kutoa harufu mbaya.
No comments:
Post a Comment