Ilikua
taarifa kubwa sana pale mtoto rubani mwenye umri wa miaka 17
alipotangaza maamuzi ya kusafiri na ndege ndogo ya injini moja kwenye
nchi mbalimbali duniani ikiwa ni ndani ya Mabara matano, vituo 25 ndani
ya nchi 15 kwenye siku 30.Haris Suleman na baba yake mzazi ambae pia ni
Rubani walichukua mafunzo mbalimbali ya kutua kwenye maji wakati wa
dharura kabla ya kuanza safari yao waliyoiandaa kwa miezi wakiwa na
lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wa familia masikini
nchini Pakistan waweze kwenda shule.
Sasa
imethibitika kwamba mtoto huyu rubani aliekua anataka kuweka rekodi ya
dunia kwa kuwa rubani mdogo aliesafiri umbali mrefu, amefariki dunia na
mwili wake kupatikana baada ya ajali ya ndege hiyo iliyotokea baharini
Jumanne usiku ambapo Baba yake ambae walikua pamoja hajulikani alipo.
Mpaka
sasa chanzo cha kuanguka kwa ndege hii hakijajulikana ambapo Hiba
Suleman ambae ni dada wa marehemu amesema ‘tunatumai baba yetu yu hai,
tutaendelea kusali mpaka tutakapopata jibu la mwisho… ‘
Wawili
hawa walikua na blog yao ambayo walikua wanapost vitu mbalimbali
zikiwemo picha za wanakopita au kutembelea ambapo post yao ya mwisho
kuiweka ilikua ni July 20 2014 Bali Indonesia.
Watu
mbalimbali waliokua wanawafatilia wameanza kutoa salamu zao za
rambirambi kwa familia baada ya kupokea taarifa za ajali waliyoipata
ambapo mmoja wa waliokua wanawafatilia ni Private Pilot Ahmed.
Ahmed
amesikitishwa na ajali waliyoipata na kusema imeuma zaidi hasa kwa
sababu ndio ilikua karibu wamalize safari hii ambayo ni rekodi ya dunia.
R.I.P Haris Suleman.
No comments:
Post a Comment