Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi katika mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu kumshitaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Dk.
Valentino Mokiwa.
Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na
kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo
ya Ilala, kimemdhalilisha.
Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba
Kanisa la
Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.
Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.
Mtikila alivyoitwa na Askofu Mokiwa ili kujadili hilo alifika na wenzake
watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa
kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nicholous, usiku wa saa 03:00.
Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na
wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna
mtu ana kinasa sauti. Baadae Askofu Mokiwa nae alisimama na kuungana na
wenzie kuwakagua kina Mtikila baada ya kuhakikisha mlango umefungwa.
Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai
kwamba operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.
Wakili wa Upande wa mashtska aliiambia mahakama kuwa, "Mlalamikiwa
alitangaza kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe na
kwamba atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola,
hakuna aliyebisha."
Alisema kisha akaendelea "Mshtakiwa (Mokiwa) alianza kupenyeza mikono
yake kwenye shingo kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa
ilionekana waziwazi ikipapasa makalio ya mlalamikaji".
Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha.
Madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko,
wasiwasi, aibu katika jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa
mara na matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.
Kesi inasikilizwa kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, chini ya Hakimu Agness Mchome.
No comments:
Post a Comment