16 July 2014

MBWANA SAMATTA NA THOMAS ULIMWENGU WATUA DAR ASUBUHI YA LEO KUWAVAA `BLACK MAMBAS`


WASHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza klabu ya TP Mazembe ya Congo, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wamewasili asubuhi ya leo tayari kuwavaa Msumbiji (Balck Mambas) jumapili ya wiki hii ndani ya dimba la Taifa.Mechi hiyo ni ya kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika, mwakani nchini Morocco na mshindi wa jumla katika mechi mbili ndiye atafuzu hatua ya makundi.
Nyota hao wametua nchini kwa  ndege ya Egypt Air wakitokea Tunisia ambapo timu yao ya TP Mazembe imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taarifa njema kwa mashabiki wa soka nchini ni kuwa washambuliaji hao wenye uzoefu na mechi za kimataifa wamewasili wakiwa fiti kwa kazi.
Samatta aliwakosa Zimbabwe mjini Harare, lakini safari hii yuko fiti na ameahidi kufanya kazi ya kulisaidia taifa katika mchezo wa jumapili.
Pia shukurani kwa TP Mazembe waliowaruhusu wachezaji hawa mapema kujiungga na wenzao, hivyo ni matarajio ya kuwaona nyota hao wakisaidiana na wenzao kuifunga Msumbiji nyumbani.
Taifa stars inahitaji ushindi wa zaidi ya magoli matatu katika uwanja wa nyumbani ili kujiweka mazingira mazuri ya kusonga mbele kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili baadaye mjini Maputo nchini Msumbiji.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi Tukuyu mkoani Mbeya ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud Ashour kutoka Misri.


Stars itarejea jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa (Julai 18 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo wakati Mambas nao wanatarajiwa kutua siku hiyo hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname