Mamlaka
ya Marekani inayoshughulikia usalama katika safari, haitoruhusu simu za
mkononi ama vifaa vingine vya elektroniki za abiria wanaoenda Marekani
kwa ndege kutoka katika viwanja vya ndege vya nchini mbalimbali duniani
kama vifaa hivyo vitakuwa havina chaji.Hatua hiyo ya mamlaka hiyo ya TSA
ilitangazwa wiki iliyopita kuboresha usalama kufuatia kuwepo taarifa
kuwa kundi la Al Qaida nchini Yemen na kundi la kiislamu la Nusra Front
lenye uhusiano na al Qaeda nchini Syria, yamepanga kulipua ndege.
Kutokana na kuwepo na hofu katika baadhi ya viwanja vya ndege duniani,
askari wa usalama wanaweza kuwataka abiria kuwasha simu zao katika vituo
vya ukaguzi na kama zikiwa hazina chaji hazitaruhusiwa kuingia kwenye
ndege.
Wataalam wa masuala hayo wanadai kuwa komputa za laptop ni miongoni mwa vitu walinzi wanaweza kuwataka abiria waviwashe.
Maafisa wa Marekani wanahofia kuwa simu za mkononi, tablet, laptop ama vifaa vingine vya elektoniki vinaweza kutumika kama bomu.
Maafisa
hao wamezitaja simu zitakazokuwa zikikaguliwa ni iPhones na Samsung za
abiria wanaotoka kwa ndege kutoka Ulaya, Mashariki ya kati na Afrika.
No comments:
Post a Comment