Klabu ya Real Madrid imeonyesha kutojutia gharama
zilizotumika wakati wa usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Colombia
James Rodriguez aliyesajiliwa juma lililopita akitokea kwenye klabu ya
AS Monaco ya nchini Ufaransa.
Real Madrid wamethibitisha kuanza kurejesha sehemu ya gharama za usajili wa mshambuliaji huyo baada ya kukiri kufanya mauzo ya jezi namba 10 ya Rodrigues kwa kiasi kikubwa.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo inaeleza kuwa, mpaka sasa jezi 345,000 za mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 zimeshanunuliwa na mashabiki wa mjini Madrid pamoja na sehemu mbali mbali ulimwenguni kote.
Mauzo yaliyofanyika yanafikia kiasi cha Euro million 33.4 ikiwa ni inakaribia nusu ya ada ya usajili iliyotumika katika uhamisho wa Rodrigues ambayo ilikuwa ni Euro million 80.
Mpaka taarifa hizi zinatolewa bado jezi ya Rodrigues ilikua inaongoza kwa mauzo, ambapo tathmini iliyofanyika inaonyesha kwa muda wa saa moja mashabiki hununua Jezi 1,000.

No comments:
Post a Comment