MSAKO wa
Fisi waliovamia makazi ya Vitongoji vitatu vya Kijiji cha Hungumalwa
Kata ya Hungumarwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, umezua maajabu.
Maajabu
hayo yamehusishwa na imani za kishirikina, baada ya fisi wawili kati ya
12 waliouawa, kukutwa wamevalishwa shanga na Rozali, kiunoni.
Msako
huo wasiku tatu ulioanza juzi(Jumapili) unahusisha mamia ya wananchi wa
Kijiji hicho na vitongoji vyake vya Mwanzabalemi, Mwanega na Mwang’ombe,
wanaotumia siraha za jadi na mbwa wapatao 50.
Habari za
ndani kutoka Kijijini humo zimesema kwamba, kabla ya wananchi hao
kuingia ‘vitani’ kusaka wanyama hao ambao baadhi wanadaiwa kumilikiwa na
watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina, wazee wa Kijiji
na Vitongoji hivyo, walifanya mazindiko (kinga) ya kujikinga na nguvu
za washirikina ambazo zinge kwamisha zoezi hilo.
Kwa
mujibu wa baadhi ya wazee wa kijiji hicho ambao hawakutaka majina yao
yaandikwe, walisema kuwa makamanda wa jadi wanaoongoza msakao huo pamoja
na mbwa wao, wana kinga za kupambana na imani za kishirikina vinginevyo
wasingeweza kuua fisi wenye shanga na Rozali wanaotumiwa kishirikina.
Diwani
wa Kata ya Hungumalwa Shija Malando akizungumza na waandishi katika
Kijiji hicho jana, alisema wananchi walifikia maamzi ya kufanya msako
huo wa siku tatu, baada ya kundi kubwa la Fisi hao wanaokadiliwa kuwa
zaidi ya 80, kuwa tishio kwa watoto na mifugo.
Alisema kuwa, kwa muda wa miaka
miwili iliyopita hadi sasa, licha ya wanyama hao kuharibu hekali moja ya
matunda aina ya Tikiti Maji yaliyokuwa yamelimwa na mwanchi mmoja,
wameua ng’ombe 109, Mbuzi 135, kondoo 127 na Nguruwe 15 katika Vitongoji
hivyo.
“Njooni muone maajabu haya.”
Alisema Malando na kufafanua “Jana (juzi Jumapili) wananchi walifanikiwa
kuua fisi kumi wawili kati yao wakiwa na maajabu. Mmoja aliukuwa na
Rozali kiunoni na mwingine akiwa na shanga kiunoni huku uume wake ukiwa
umetahiriwa kama binaadam.”
Alisema fisi waliokutwa na vitu
hivyo kiunoni, kwa imani za kabila la Kisukuma, wanadaiwa kumilikiwa na
baadhi ya watu wenye imani za kishirikina na kwamba, waliuawa majira ya
saa 8 hadi saa 10 mchana kwenye eneo la mlima wa Mwanzabalemi.
Alifafanua kuwa, fisi kumi waliuawa
(jumapili) siku ya kwanza ya msako huo na wengine wawili waliuawa jana
asubuhi na kwamba maeneo ya milima ya Mwanangi katika Kijiji cha Buyobo
na Kitongoji cha Mwanzabalemi yanasadikiwa kuwa na fisi wengi zaidi.
“Pamoja na kushambulia mifugo wetu,
ilifika mahali wananchi walikuwa hawawezi kutembea kwa uhuru nyakati za
usiku na baadhi ya watoto wanaosoma mbali kukatisha masomo kwa kuhofia
kuliwa na fisi hao.” Alieleza Mwenyekiti wa Kijiji cha Hungumalwa,
Clement Kaswahili.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Mwang’ombe Joseph Kisena alisema hadi kufikia leo (siku ya tatu ya msako
huo) watakuwa wameua fisi wengi zaidi kutokana na ushirikiano mzuri wa
Vitongoji hivyo vinavyotumia mbwa 50 na siraha mbalimbali za jadi
ikiwemo mikuki, mapanga na marungu.
Kisena alisema, pamoja na maajabu
ya fisi kuvaa shanga na Rozali kiunoni ambayo wamejionea na kuzua imani
za ushirikina kwa baadhi ya wananchi, hawatarudi nyuma, hadi
walitokomeze kundi la wanyama hao ambalo ni tishio kwa wananchi na
mifugo wao.
No comments:
Post a Comment