Arafa Mohammed Mke
wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete(kushoto)
akimkabidhi zawadi ya Vyombo vya ndani na Tende mzee Said Khamis Mnyika
wa kijiji cha Changarikwa kata ya Mbwewe kama zawadi ya mbunge huyo
katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa familia zenye mahitaji muhimu
kutokana na kiushi katika mazingira magumu , ambapo vifaa vya ndani
pamoja na Tende zitatolewa kwa familia zipatazo 600 katika kata zote za
jimbo hilo, huu ni mwendelezo wa shughuli za mbunge huyo katika
kuwatumikia wapiga kura wake na kuboresha maisha yao ikiwa ni mikakati
yake ya kufikia malengo aliyojipangia kwa kushirikiana na wananchi wa
jimbo la Chalinze, Kulia ni Mzee Ahmad Ramadhan mmoja wa wazee wa kijiji
cha Changarikwa akingoja kukabidhiwa zawadi zake .(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBWEWE-CHALINZE)
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete(kushoto) akimkabidhi zawadi ya vyombo vya ndani na Tende Mzee Ahmad Ramadhan mmoja wa wazee wa kijiji cha Changarikwa wakati alipotoa zawadi hizo kwa familia zenye mahitaji muhimu katika kata ya Mbwewe jana.
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi zawadi hizo Bi.Halima Hassan katika kijiji cha Changarikwa jana.
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na wazee wa kijiji cha Kwaruhombo Kata ya Mbwewe
jana baada ya kuwakabidhi zawadi ya Tende,Wa pili kutoka kushoto ni
rehema Zando Diwani viti maalum Bagamoyo.
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi aliowakabidhi zawadi
hizo, baadhi ni viongozi wa kata hiyo na wilaya ya Bagamoyo.
Mzee Said Khamis Mnyika kushoto na Mzee Ahmad Ramadhan wa kijiji cha Changarikwa wakiwa na zawadi zao mara baada ya kupokea kutoka kwa Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete jana.
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akipanga
vifaa mbalimbali kwenye ofisi ya CCM kata ya Mbwewe kabla ya
kuvikabidhi kwa familia za watu wenye mahitaji muhimu jana.
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi zawadi ya vyombo vya ndani na Tende Bw. Abdulrahman Juma wa Mbwewe.
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi zawadi hizo Mlemavu Halia Saleh.
Baadhi ya akina mama wakiwa na zawadi zao mara baada ya kukabidhiwa
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi aliowakabidhi zawadi,
wengine ni baadhi ya viongozi wa kata hiyo na wilaya ya Bagamoyo.
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza mmoja wa akina mama waliopokea zawadi hizo wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa Mh. Mbunge Ridhiwani Kikwete.
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akihojiwa
na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha kazi ya
kugawa zawadi hizo kwa baadhi ya familia zinazoisi katika mazingira
magumu
No comments:
Post a Comment