WAKATI
hamu ya mashabiki kila kona kwa sasa ni Agosti 8, mwaka huu katika
tamasha kubwa la kihistoria la Usiku wa Matumaini litakalofanyia Uwanja
wa Taifa jijini Dar, mashabiki wengi wanatamani kuwaona wakali kibao
wakipanda jukwaani na kupiga nyimbo zao kali.
Good newz ni
kwamba Zuwena Mohamed ‘Shilole’ atapanda jukwaa moja na diva wa muziki
kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade kudondosha shoo
ya kihistoria.
Uzuri wa wasanii hao wawili ndiyo unashawishi watu wengi kufika katika tamasha hilo lenye lengo ya kuchangia mfuko wa elimu nchini. Unataka kujua sifa za wasanii hao? Hizi hapa:
Uzuri wa wasanii hao wawili ndiyo unashawishi watu wengi kufika katika tamasha hilo lenye lengo ya kuchangia mfuko wa elimu nchini. Unataka kujua sifa za wasanii hao? Hizi hapa:
Shilole
ambaye wengi wamezoea kumwita Shishi Baby, amekuwa habahatishi
jukwaani kwa jinsi anavyojua kuwapagawisha, hivyo mashabiki wategemee
sapraizi kibao kutoka kwa bidada huyo kwenye sekta maalum ya kukata
mauno na kuacha watu midomo wazi.
Kwa
upande wake, Yemi Alade anatisha balaa. Staili ya Johnny ndiyo
atakayoinesha siku hiyo huku akichungulia kwa kumtafuta Johnny uwanjani
mpaka atakapofanikiwa kumuona na kurudi naye Nigeria kama alivyoahidi.
NGOMA ZAO
Pata picha kwa Shilole atapopanda na kupiga nyimbo zake kali kama Chuna Buzi, Lawama, Nakomaa na Jiji, Paka la Baa na Namchukua inayotamba kwa sasa, hakika patakuwa hapatoshi kwani Shilole amesema hatabakisha kitu siku hiyo.

Bidada
Yemi Alade atashuka na ngoma inayotamba Afrika, Johnny kisha
atazidondosha kali nyingine ambazo zimetokea kuiteka Afrika kama
GhenGhenLove, Bamboo, Show Me na Tangerine.
MADANSA
Shilole ameahidi kudondoka na madansa wake ambapo watakuwa naye sambamba jukwaani katika kukamua siku hiyo.
Shilole ameahidi kudondoka na madansa wake ambapo watakuwa naye sambamba jukwaani katika kukamua siku hiyo.
“Mashabiki
wategemee kuona mpangilio na staili tofauti kutoka kwa masteji shoo hao
ambazo zitakuwa funika bovu,” alisema Shilole.
Yemi
naye hatakuwa nyuma katika eneo hilo, ameahidi kucheza sambamba na
madansa wake siku hiyo. Kama ilivyo kwenye makamuzi yake kupitia video
ya Johnny na Tangerine ambapo madensa wake wanaonekana wakikamua mwanzo
mwisho.
WENGINE
Mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto amefunguka kuwa mbali na shoo hiyo kali, utamu zaidi utakolezwa zaidi na mastaa wakali wa Bongo Fleva wakiongozwa na mfalme, Saleh Ally ‘Ali Kiba’, Meninah, Madee, R.O.M.A Mkatoliki, Scorpion Girls, Juma Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi.
“Kila msanii atakayepanda jukwaani atahakikisha anapiga nyimbo zake zote ndipo ampishe mwenzake, itakuwa ni jiwe baada ya jiwe,” alisema Maloto.

Aidha,
tamasha hilo litapambwa na mechi za mpira wa miguu kati ya wabunge
mashabiki wa Simba na wenzao wa Yanga, Bongo Fleva na Bongo Movie pamoja
na mapambano kibao ya ndondi, burudani zote hizo mashabiki watazipata
kwa kiingilio cha shilingi elfu tano.
Tamasha hilo limedhaminiwa na E.FM, Clouds FM, Times FM, Vodacom, Pepsi, Azam TV na SYSCORP.
No comments:
Post a Comment