Dida Shaibu, mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani
amefunguka Exclusively kupitia Sunrise ya 100.5 Times Fm inayoongozwa na Fadhili Haule na kueleza
chanzo cha ndoa yake na Ezden ‘The
Rocker’
Jumanne kuvunjika. Ndoa iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja tu.
Jumanne kuvunjika. Ndoa iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja tu.
Dida ameeleza kuwa mzizi wa tatizo lililopelekea ugomvi
mkubwa kati yao ni
simu ya mkononi ya mumewe huyo wa wazamani baada ya kutaka
kuitumia kucheza game na kugundua kuwa imewekewa password kwa mara ya kwanza
katika uhusiano wao.
“Tatizo kubwa la ugomvi wangu na X-Husband, tatizo kubwa
lilikuwa ni simu. Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumatano tumetoka kazini. Tukawa
tuko kawaida, unajua sisi huwa tunataniana sana. Kwa hiyo aliacha simu yake
kitandani, unajua mimi huwa nacheza game kupitia simu yake. Kwa hiyo mimi
nikachukua simu yake nikakuta ameweka password kitu ambacho sio cha kawaida.
Kwa hiyo mimi ikabidi nimuulize…nikamuita, tulikuwa tunaitana ‘mshikaji wangu
mshikaji wangu’. Kwa hiyo alikuwa yuko bafuni anaoga, kwa sababu nyumba ni
self-contained, kwa hiyo nikawa namwambia ‘duh mshikaji wangu mbona umeweka
password?’ yaani kama utani tu, akaniamba ‘aah we iache simu yangu’.” Dida
ameiambia Sunrise ya Times Fm.
Wanandoa washikaji, Dida na Ezden (December, 2013)
Amesema Ezden alishikilia msimamo wake kutomuonesha password
kitu ambacho kilimpa hisia na wasiwasi kuwa huenda jamaa anamsaliti
(anamichepuko) ameficha kupitia simu hiyo na kuanza kuongeza nguvu ya kuomba
apewe password ili aondoe wasiwawasi wake lakini hakufaulu zoezi hilo.
Ameiambia Sunrise ya 100.5 Times Fm kuwa kitu kilichomfanya
afikirie kuwa ameonewa kwa kunyimwa password ni uhuru aliokuwa nao mumewe huyo
wa zamani kupitia application za kidijitali.
Amesema Ezden alikuwa na uwezo wa kuona kila kinachofanyika
kwenye simu ya Dida hata kupata jumbe
zinazoenda kwenye simu ya Dida kabla mwenyewe hajazipata.
Dida na Ezden wakifunga ndoa July,2013
“Simu yangu anauwezo wa kushika akakaa nayo, simu yangu
anaweza kushika akadownload vitu vya kuweza kufatilia Dida anaenda wapi, Dida
anafanya nini. Messages zangu za WhatsApp alikuwa anaweza kupata yeye kabla
yangu mimi. Na kingine kikubwa ni kwamba alikuwa anaweza kudownload maongezi
ambayo naongea na watu. Lakini hajawahi kukuta maongezi mabaya na watu….Nikiwa
Kawe simu yake inamuonesha kuwa Dida yuko Kawe.” Ameeleza.
Hata hivyo, ametaja kuwa wasiwasi wa mumewe huyo wa zamani
na mabadiliko yake katika matumizi ya simu yalitokana na ujumbe ambao alikuwa
ametumiwa na mwanaume ambaye kwake yeye ni mteja.
Lakini ujumbe huo haukueleweka vizuri kwa sababu kuna kitu
anadhani kilimiss kwenye ujumbe huo kilichosababisha ieleweke tofauti (Kama mtu
anaechepuka nae).
Ameeleza kuwa alipoendelea kuomba zaidi password na hali ya
kutoelewana kuongezeka akajikuta akipigwa vibao na hapo mambo yakazidi kuwa
mabaya kwenye uhusiano huo.
“Alinipiga kibao, sio kibao tu, Vibao vya uhakika….baada ya
kupigwa mimi nilishikwa na hasira kwa sababu alinipiga na baadae akaona kibao
hakitoshi. Akachukua mkanda, mkanda huu wenu wa suruali lakini ulikuwa mzito
akawa ananichapa nao ‘kwa nini unataka kupishika vitu vyangu’.
Anasema kutokana na kipigo hicho aliumia kichwani na
kuelekea hospitali, lakini aliporudi nyumbani alikuta mwenzake ameshachukua
vitu vyote alivyokuwa anavimiliki (alivyoenda navyo).
Alipoulizwa nani alimuacha mwenzake:
“Sitaki kusema nani kamuacha mwenzake kwa sababu mimi ndiye
niliomba divorce. Katika maisha ya mwanadamu wanasema mwanamke hauwezi kumuacha
mwanaume ila mwanaume anaweza kumuacha mwanamke. Lakini mimi nahisi kama
tumeachana.”
Katika hatua nyingine, Dida aliulizwa kuhusu mpango wake wa
baadae katika uhusiano wake kama ana mpango wa kuolewa tena. Alisema hana mpango huo kwa sasa.
“Kwa sasa sina mpango wowote wa kuhusiana na suala la ndoa.
Yaani sina na sitegemei. Na kama kuna mtu anafikiria kwa sababu napata maombi
mengi sana. Washindwe na walegee. Kwamba labda naweza kusema mwenyezi Mungu
amenijalia kuwa nabahati hiyo…Sio kupendwa yaani tuseme, unajua binadamu
anakupenda mwingine anakujaribu. Sasa hivi watanifuata wanaume wengi sana kila
mmoja atakuja kwa sampuli anayoijua yeye. Huyu atajifanya yeye ndiye ana mahaba
kuliko Yule. Mwingine anasema ‘atapigaje mwanaume?’ kumbe yeye ndiye
mdundindaji kwelikweli kuliko hata yule.
“Sitaki kuja kujutia maisha yangu, sitaki kuja kujutia
maamuzi yangu. Huwa nafanya kitu kwa kuangalia mbele zaidi. Mimi nina biashara
zangu, nina maisha yangu. Namshukuru Mungu amenijalia mtoto mmoja. Kwa hiyo
nahitaji mtoto wangu awe na maadili fulani hivi ambayo ya kusema kwamba huyu ni
mama..nahitaji kumsomesha, nahitaji awe hivi. Lakini sitaki mwanangu asipate
matatizo haya ambayo labda mama yake nimepitia. Lakini hii yote nasema ni
ujasiri. Nasema Mwenyezi Mungu labda ananionesha njia.”Chanzo Timesfm.co.tz
No comments:
Post a Comment