CHRIS BROWN HATARINI KUUAWA NA MAJIRANI ZAKE...SOMA ZAIDI HAPA

Mwimbaji
wa Loyal, Chris Brown ambaye alitoka jela hivi karibuni na kuamua
kutafuta amani kwa kuhama nyumba aliyokuwa akiishi kukwepa ugomvi na
majirani zake ni kama ameruka majivu na kukanyaga moto.
Kwa mujibu wa TMZ, mwimbaji huyo aliamua
kuuza nyumba yake ya kifahari iliyokuwa Hollywood Hills kufuatia ugomvi
wa kila siku na majirani zake waliomfikisha kwenye vyombo vya sheria
mara kadhaa kwa madai ya kuwanyima raha na familia zao kwa vitendo
vyake. Baada ya kuuza nyumba hiyo alinunua nyumba mpya, California.
Kwa bahati mbaya majirani wapya wa
mwimbaji huyo wanaonekana kuwa na maamuzi magumu zaidi ya wale wa awali
waliokuwa wanampeleka kwenye vyombo vya sheria.
Akiongea na TMZ,
jirani mmoja alieleza kutofurahishwa kwake na ujio wa Chris Brown kwenye
ujirani wao na kuahidi kuwa endapo atagusa nyumbani kwake atampiga
risasi.
“It can be the devil. I can care less.. I don’t care if
they are having orgies. It can even be Sadam Hussein for all I care, as
long as he doesn’t trespass onto my property. If he does, I shoot him.” Jumba jipya la Chris Brown lina vitu vya
kifahari kama uwanja wa kuchezea tennis, dance studio, club house,
commercial ice cream bar na mengine mengi huku eneo zima likuwa na
ukubwa wa eneo la mraba futi 8,000 na vyumba sita vya kulala
No comments:
Post a Comment