Jina la Tanzania
linameremeta wakati wanamichezo wetu walipopita katika maandamano ya
ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye sherehe kabambe za
ufunguzi katika Uwanja wa Celtic Park jijini Glasgow, Scotland, uliobeba
watazamaji 40,000 huku watu bilioni 1 wakiangalia live sherehe hizo
kupitia katika TV zao. Takriban mashabiki
100,000, na wanamichezo 4,000 kutoka katika nchi 71 zitakazoshindana
wapo hapo kwa michezo hiyo ambapo hii ni mara ya 20 kufanyika toka
ianzishwe.
Sehemu ya wanamichezo wa Tanzania kwenye sherehe hizo za ufunguzi. Jumla
ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni
jitihada za Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini
kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali
wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za
Uturuki, China na New Zealand
Tanzania Oyeeeee....!!!!
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Suleiman Mjaya Nyambui (T-shirt ya njano) akihamasisha vijana wake
Nahodha na bondia wa
Tanzania Seleman Salum Kidunda akipeperusha juu bendera ya Taifa wakati
akiongoza wenzake kwenye maandamano hayo ya ufunguzi.Chanzo Issamichuzi
Blog
No comments:
Post a Comment