Usiku wa kuamkia jana Mario Balotelli alipiga hatua moja mbele kwenda kuhalalisha mahusiano yake na mrembo Fanny baada ya kumchumbia rasmi.
Balotelli alitumia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kuwaambia mashabiki na rafiki zake kwamba Fanny amekubali kuolewa nae.
Baada ya muda kidogo mrembo Fanny nae akatumia akaunti yake ya Instagram kuonyesha pete aliyovalishwa na Balotelli.
No comments:
Post a Comment