12 June 2014

NDEGE ZA 'MALAWI' ZINAZOVINJARI ZIWA NYASA ZATAJWA BUNGENI, KUMBE ZINATOKEA DODOMA


 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
Habari zilizopatikana hivi punde kutoka bungeni Dodoma  ni kwamba ndege tatuzinazovinjari upende wa Tanzania katika Ziwa Nyasa ni za Tanzania zilizokodiwa na Serukali ya Malawi kwa ajili ya utafiti wa kijiolojia.
Taarifa hiyo imetolewa ma Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, bungeni Dodoma asubuhi hii, baada ya Mbunge wa Ileje, Aliko Kibona kuitaka Serikali kutoa taarifa sahihi juu ya suala hilo, kwani zimekuwa zikiwatia hofu wananchi waishio mpakani na Malawi.

Amesema kuwa ndege hizo zimekodiwa  kutoka Dodoma Tanzania na kwamba zimepata vibali vyote kutoa  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Mwakyembe, amewapongeza Watanzania kwa kuwa na uharaka wa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa jambo lolote wanalolitia wasiwasi kama hilo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname