Bao
la dakika za lala salama: Haris Seferovic aliifungia Uswisi bao la
dakika ya mwisho na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ecuador.
Switzerland
ikitoka nyuma imefanikiwa kuitandika Ecuador mabao 2-1 katika mchezo
wao wa ufunguzi wa kundi E kombe la dunia mjini Brasilia.
Admir
Mehmedi aliyedumu uwanjani kwa sekunde 121 aliifungia Uswisi bao la
kusawazisha baada ya Enner Valencia kuifungia Ecuador bao la kuongoza.
Baol la Seferovic limehakikisha kuwa hakuna sare katika michuano ya mwaka huu, kwa mara ya kwanza tangu 1934.
Seferovic akishangilia bao
Wachezaji wa Uswisi walijiunga na mshambuliaji huyo kushangilia bao hilo la ushindi.
No comments:
Post a Comment