Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi.
Imeelezwa Flora na mumewe ambao
walifunga ndoa Agosti 22, 2002 wamepita katika migogoro mizito lakini
wawili hao walikuwa wakiyamaliza kifamilia hadi kufikia hili la hivi
karibuni ndilo lililoziba mataumaini ya wawili hao kuishi kama mume na
mke.
Chanzo kilicho karibu na wawili hao
kimeeleza kuwa, mzizi wa wawili hao kugombana ulichochewa na mwanamke
mmoja (jina tunalo) ambaye alikuwa akikinzana na ushauri wa Mbasha mara
kwa mara.
“Kuna vitu Mbasha alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili na hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagana,” kilisema chanzo.
“Kuna vitu Mbasha alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili na hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagana,” kilisema chanzo.
TUJIUNGE NA MBASHA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Emmanuel alizungumza na mwandishi wetu ambapo alikiri ndoa yake haina uhai tena na si rahisi kurejea katika hali ya kawaida licha ya kudai kuwa bado anampenda mkewe.
“Tulikuwa tunagombana sana na Flora lakini tulikuwa tukipatana ila mama… (anamtaja jina) alichangia ugomvi,

Flora naye alikuwa na nyendo zake
mbaya, kuna wakati alikuwa anatoka kwenda gym (sehemu ya mazoezi)
anachelewa kurudi ikafika wakati na nguvu ya ndugu wa mke ikawa kubwa
kiasi cha kunizidi mimi na hapo ndipo mambo yalipofikia pabaya kabisa.”
FLORA ATIMKA NYUMBANI
Mbasha anaendelea: “Ugomvi ulizidi, ilifika wakati tulipishana kiasi cha yeye kuondoka nyumbani na kwenda kuishi katika nyumba ya wageni kwa miezi kadhaa wakati huo.
Mbasha anaendelea: “Ugomvi ulizidi, ilifika wakati tulipishana kiasi cha yeye kuondoka nyumbani na kwenda kuishi katika nyumba ya wageni kwa miezi kadhaa wakati huo.
“Ndani ya ugomvi huo nilisikia mengi,
baadhi ya watu wananiambia mke wangu anaonekana na Prado na mwanaume
mwingine mwenye pesa, iliniuma sana ingawa sijawahi kumuona moja kwa
moja,” alisema Emmanuel.
“Mimi sina tatizo kabisa na mume
wangu, nimeshasamehe yote yaliyopita, kuhusu mashitaka ningeweza
kuyafuta kama ningekuwa mimi ndiye niliyemshitaki,” alisema Flora.
FLORA ADAIWA KUHAMIA KWA GWAJIMA
Wakati gazeti hili likiendelea kusaka undani juu ya sakata hili, kuna chanzo kingine kilipenyeza data kuwa baada ya ugomvi kuwa mzito, Flora alihamia kwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar, Josephat Gwajima ambako ndiko alikuwa akisali kila Jumapili.

“Kwani nyinyi Global hamna habari?
Flora amehamia kwa Gwajima Jumapili iliyopita, kwanza alihudhuria ibada
jioni akaenda kuishi maana Gwajima ni mchungaji wake kwa sasa,” kilisema
chanzo.
GWAJIMA ACHOMOA
Ili kupata mizani ya madai hayo, juzi Amani lilimpigia simu Mchungaji Gwajima na kumuuliza kama kweli Flora amehamia kwake kufuatia ugomvi kati yake na mumewe ambapo alikataa katakata.
“Flora hayupo hapa…mnataka niwaambiwe yuko hapa halafu vyombo vya habari muanze kuandika vibaya? Hakuna kitu kama hicho,” alisema Gwajima.

KWA NINI CHALI?
Ndoa kuwa chali ni ile ambayo imeanguka lakini inaweza kusimama tena tofauti na ndoa kuvunjika. Global iliwahi kuandika NDOA YA THEA CHALI baadaye ikasimama tena. Thea ni msanii wa filamu alifunga ndoa na Michael Sangu ‘Mike’ ambaye pia ni mwigizaji.

Wakati Emmanuel akizungumza na
mwandishi wetu, alikiri kuwa Flora ameshamgeuka na nguvu kubwa
imemuingia ndani ya moyo wake hivyo kuna ugumu sana wa kurudiana.
“Flora ambaye nilitegemea awe msaada
katika hili lakini amefikia steji ya kuacha kunisikiliza, anasema
haniamini, kwamba ninaweza kumfanyia lolote, sasa si bora kama anataka
tuachane kwa heri kuliko kuniundia zengwe ambalo linataka kunipeleka
mimi jela?” alihoji Mbasha.
Kutokana na mvutano huo pamoja na
kesi hiyo ya kudaiwa kubaka inayomwandana Mbasha ni dhahiri kwamba kila
mmoja hana imani na mwenzake tena hivyo suala la wawili hao kuishi kama
zamani linakuwa gumu kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Emmanuel Mbasha alishitakiwa katika
Kituo cha Polisi cha Tabata Shule, Mei 30, mwaka huu kwa madai ya
kumbaka shemejie.Uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea hadi sasa
shitaka ambalo mwenyewe amelikanusha
No comments:
Post a Comment