HATIMAYE familia ya denti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, marehemu Sekabenga Pius Mwakimenya (21) kilichotokea hivi karibuni na kugubikwa na utata, imeanika ukweli kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza na Uwazi, mwishoni mwa wiki iliyopita katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, baba mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina
la Joseph Mwigune alisema, taarifa waliyopewa na daktari aliyemfanyia uchunguzi
inamaliza utata na minong’ono yote inayoendelea chuoni.
Alisema, kwa mujibu wa ripoti hiyo, kifo cha Sekabenga
kimetokana na mzunguko wa damu katika mishipa kutokuwa sawa, jambo
lililosababisha ajisikie vibaya na hatimaye kufariki dunia.“Daktari amesema
kwamba mishipa ya damu haikuwa ikifanya kazi vizuri hali iliyomsababishia
ajisikie kuchoka kwa sababu damu haikuwa ikifika sehemu zote za mwili wa
marehemu,” alisema Mwigune.
Uwazi lilifunga safari hadi chuoni na kuzungumza na baadhi
ya wanafunzi ambao walionyesha wasiwasi kuwa huenda marehemu aliamua kujiua kwa
sumu kwa maelezo kuwa, siku chache kabla ya kifo chake alionekana mwenye mawazo
mengi.
“Hakuwa mwenye furaha, ni kama alikuwa na jambo zito
linalomsumbua ndiyo maana unasikia wanafunzi wengi hapa chuoni wanahusisha kifo
chake na sumu,” alisema denti mmoja kwa sharti la kutotajwa jina lake.Hata
hivyo, taarifa kutoka kwa familia inayonukuu ripoti ya daktari inaziba minong’ono
yote kwa kuwa haionyeshi mahali popote kuwa marehemu alijiua kwa sumu.Marehemu
Sekabenga alikuwa mwaka wa pili chuoni hapo
akichukua Shahada ya Kwanza ya Biashara na Uhasibu, mwili wake umesafirishwa Jumamosi Mei 31, mwaka huu
kwenda mkoani Mbeya kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika jana Jumatatu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina.
Chanzo:gazeti la uwazi
No comments:
Post a Comment