Mfanyabiashara
wa madini, Richard Lucas (29) anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi
kichwani baada ya kusababisha ajali mbili tofauti. Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema alijipiga risasi juzi saa 12:45
jioni nyumbani kwake eneo la Kimandolu. Alitumia bastola aina ya Luger
yenye namba B136986 . Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa
Lucas alitokea Tengeru akiwa na gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba
za usajili T 494 CKY alikokuwa amemfuata rafiki yake aliyekuwa amepata
ajali ya kugongwa na gari.
Alipofika
eneo la Sekei Darajani, alimgonga mwendesha pikipiki na kuendelea na
safari. Mbele kidogo, kwa mujibu wa polisi, aligonga daladala lenye
namba za usajili T 636 CUR aina ya Nissan iliyokuwa inachukua abiria.
Baada ya hapo gari ya Lucas ilipinduka na waliokolewa kwa kupitia dirishani na wananchi.
Inadaiwa
alitoka eneo la tukio kwa pikipiki ya kukodi kwenda nyumbani kwao
Kimandolu huku akimwacha Vick Mchuma kwenye eneo la tukio.
Alisema
baada ya muda, Mchuma ambaye waliongozana naye kwenda kumsaidia rafiki
yao aliyepata ajali Tengeru, alipata taarifa kuwa Lucas amejipiga risasi
na mwili upo Hospitali ya Mount Meru. Polisi wanaendelea na uchunguzi
wa tukio hilo.
Wakati
huo huo, polisi imetoa taarifa ya kifo cha mpanda mlima, Denis Joeli
aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali chini ya bega la kulia
karibu na moyo alipotofautiana na mtu aliyekuwa akimdai Sh 40,000.
Kamanda Sabas alisema tukio hilo ni la juzi saa 8:30 asubuhi kwenye kitongoji cha Olturei-Moivo wilayani Arumeru.
Alisema
uchunguzi wa awali wa polisi umebaini Denis alichomwa na Solomon
Lembris, waliyetofautiana kauli wakati wakidaiana fedha.
No comments:
Post a Comment