14 June 2014

MASHABIKI WAMTAKA BI. CHAU AKAE EDA KUFUATIA KIFO CHA MZEE SMALL, MHHHH... SOMA ZAIDI HAPA!


Muigizaji mkongwe Chausiku Salum ‘Bi Chau’.

MUIGIZAJI MKONGWE CHAUSIKU SALUM ‘BI CHAU’ AMESHANGAZWA NA DHANA ILIYOPO KWA MASHIBIKI KWAMBA YEYE NI MKE WA MAREHEMU SAIDI NGAMBA ‘MZEE SMALL’ HUKU WAKIMTAKA AKAE EDA.

Akipiga stori na paparazi hivi karibuni, Bi. Chau alisema amekuwa akipokea simu nyingi zikimuuliza anakalia wapi eda ili wakampe pole huku wengine wakihoji kwa nini atembea mtaani wakati amefiwa.


Marehemu mzee Small akiwa na Bi Chau enzi za uhai wake.
“Baada ya mazishi nilipata wakati mgumu, nilipokuwa nikienda kazini ITV nilichukua Bajaj lakini nilipokelewa na maneno makali ambapo niliambiwa sisi wasanii ni wabaya sana, nimeona kafariki hata siku hazijaisha nimepaka piko na sijakaa eda, nilijisikia vibaya kwani Small hakuwahi kuwa mpenzi wangu,” alisema Bi. Chau.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname