14 June 2014

LORI LA MAFUTA LALIPUKA MBEYA

Lori la kusafirisha mafuta likiwa na shehena kubwa ya mafuta aina ya Diesel limeteketea kwa moto baada ya kupata ajali ya kugongwa na lori lingine katika eneo la igurusi wilayani mbarali.
 Ajali hiyo imetokea  ikihusisha lori lenye namba za usajili t 417 ABF, mali ya kampuni ya Camel oil ambalo lilikuwa likisafirisha lita 35,000 za mafuta aina ya diesel kutoka jijini Dar es salaam kwenda nchini Congo DRC ambalo linadaiwa kugongwa na lori lingine.
Baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia ajali hiyo  wameitaka serikali kuwalazimisha wamiliki wa malori kuhakikisha magari yao yanakuwa na madereva wa akiba kwa kuwa wanaamini kuwa ajali hiyo imesababishwa na dereva wa lori moja wapo kusinzia wakati akiendesha gari kutokana na uchovu wa safari ndefu.
Mpaka napata hizi habari hizi na chanzo kinatoka katika hilo la ajali, bado lori hilo lilikuwa likiendelea kuteketea huku kukiwa hakuna msaada wowote wa kuuzima moto huo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname