Kwa mara
ya kwanza katika historia, sala na mafundisho kutoka kwenye Quran
yatasikika Vatican Jumapili, ambako ni makao makuu ya kanisa katoliki
duniani.
Uamuzi huo umefanywa na Papa Francis ikiwa ni hatua ya kutengeneza mazingira ya amani kati ya waisrael na wapalestina.
Kiongozi
huyo wa kanisa katoliki duniani aliwaalika rais, Shimon Peres na rais wa
Palestina Mahmoud Abbas kwenda Vatican pale alipozitembelea Palestina
na Israel hivi karibuni.
Kwa
mujibu wa Times of Israel, marais wote wawili wamekubali mualiko huo.
Msemaji wa ikulu ya Israel ameeleza kuwa watasindikizwa na viongozi wa
dini za kikristo na kiislam.
Kwa mujibu wa Associated Press, Papa Francis amesema kuwa kutakuwa na maombi ya jioni jumapili hiyo pale watakapokutana na kwamba yatalenga kusaidia amani kati ya matakwa ya wapalestina na waisrael katika nyanja zote
No comments:
Post a Comment