14 June 2014
FLORA MBASHA AWAGAWA WACHUNGAJI...BAADHI YAO WADAI HAWAWEZI KUHUDUMIWA NA MWIMBAJI MZINZI
Mpasuko wa ndoa ya wasanii wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha na mkewe Florah umewagawa wachungaji wa makanisa mbalimbali nchini baada ya kibao kumgeukia Flora kwamba ndiye anadaiwa kusuka mpango wa kumwangamiza mumewe ili afungwe kwa kosa la ubakaji…..
Wakizungumza na wanahabari wetu kwa nyakati tofauti, wachungaji hao walisema endapo itabainika ni kweli Flora ameshiriki kumsaliti mumewe kwa kutembea na mmoja wa wachungaji maarufu nchini hapatakuwa na haja ya kumwalika kwenye huduma zao kwani hawawezi kuhudumiwa na mwimbaji mzinzi.
Mchungaji Ambonile Mwakipesye na Amani Joseph wa makanisa ya Tanzania Assemblies of God ( TAG) walisema kuwa kama kulikuwa na matatizo kwenye ndoa yao walipaswa kuwaona watumishi wa Mungu na kusuluhisha badala ya kutengenezeana mitego na kuingizana majaribuni kama inavyodaiwa kutokea kwa Mbasha….
Wakati wachungaji hao wakisema hivyo, mchungaji Thomas Methew yeye alisema kuwa ukweli wa jambo hilo wanaujua wanandoa wenyewe kwani mpaka sasa hakuna anayelijua tatizo kubwa mpaka wakafikia hatua ya kutengana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment