Kiungo kutoka nchini Hispania Cesc Fabregas amesema kabla
hajafanya maamuzi ya kujiunga na klabu ya Chelsea, bado alikuwa na
matarajio makubwa ya kurejea kwenye klabu ya Arsenal ambayo ilikubali
kumuuza mwaka 2011 kuelekea FC Barcelona.
Fabregas, aliweka wazi matarajio yake ya kurejea Emirates Stadium,
akiwa mbele ya vyombo vya habari huko nchini Brazil ambapo amedai kwamba
klabu ya Arsenal ilikuwa chaguo lake la kwanza baada ya kuthibitishiwa
hayupo kwenye mipango ya meneja mpya Luis Enrique.
Amesema alifanya mazungumzo na meneja wa klabu hiyo ya kaskazini mwa
jijini London, Arsene Wenger, kwa lengo la kutambua kama angekuwa tayari
kumrejesha, lakini alijibiwa nafasi yake klabuni hapo haipo kwa sasa.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema Wenger, alimwambia kwa
sasa nafasi yake imeshikwa na kiungo kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil
ambae alimsajili kutoka Real Madrid mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2013-14.
No comments:
Post a Comment