Mshiriki wa shindano la kuimba la Bongo Star Search (BSS) , Wababa amewatuhumu maswaiba wa ‘Muziki Gani’ Nay wa Mitego na Diamond Platinumz kwa kumuibia kazi zake kwa wakati tofauti.
Akiongea kupitia Friday Night Live ya East Africa TV, Wababa amesema Diamond amemuibia wimbo wake ambao alikua anaiita ‘Kitorondo’ na kwamba aliibadilisha jina baadae.
“Kiukweli kuhusu Diamond, mimi mwenyewe nimetumiwa hiyo ngoma ambayo ameitoa, nimeiskiliza jinsi ilivyo kuanzia idea, mwendo, style ambazo anafanya. Ambayo ameibadilisha jina tu baada ya ya kwamba ilikuwa mitandaoni nilikuwa nimemfatilia ilikuwa inaitwa Kitorondo mwezi mmoja kama uliopita. Kwa hiyo nilishindwa kulalamika kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa analalamika kuwa imevuja. Kwa hiyo sikuona sababu ya kuongea kitu kwa sababu haikuwa official. Kwa hiyo sikuwa na sababu ya kucomplaini kwa sababu haikuwa official, lakini mpaka jana ina maana ilikuwa serious kama biashara.” Ameeleza Wababa.
Wababa |
Kwa upande mwingine, Wababa amedai kuwa alifanya kazi na Nay wa Mitego katika studio za Mazoo lakini baaadae Nay alirudi studio na kuongea na Mazoo kutaka kuunua wimbo huo kwa shilingi milioni moja bila kumshirikisha Wababa.
“Hivi karibuni nimefanya ngoma mpya na Nay wa Mitego, ni ngoma ambayo ilikuwa iko paid kwake pamoja na studio. Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba siku mbili baada ya kufanya kazi nikapigiwa simu na producer akaniambia kwamba jamaa amerudi tena kwa ajili ya kutaka kununua wimbo kwa milioni moja, auchukue wimbo aende akaufanye sehemu nyingine. Baada ya hapo hata mahusiano yangu na mshikaji yamekuwa sio mazuri. Ukimpigia simu anakwambia yuko busy kuna kazi anafanya atanicheki, hadi kufikia leo sielewi.”
Nay alipigiwa simu lakini hakuwa anapatikana kwa muda huo
No comments:
Post a Comment