Mchezaji
wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez alipewa adhabu ya kutojihusisha
na soka kwa muda wa miezi minne kutoka sasa baada ya kuthibitika
kumng’ata mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini kwenye mechi za kombe la
dunia.
Pamoja
na kwamba Suarez mwenyewe amesema hakufanya hivyo makusudi na kuwa hiyo
ni kawaida kwenye matukio yanayotokea uwanjani, alipewa adhabu hiyo
kali ambayo pia imepingwa na mashabiki mbalimbali waliompokea ambao
wanaamini kaonewa.
No comments:
Post a Comment