15 June 2014

Ally Kiba Afunguka Baada Ya Kukaa KimyaKwa Miaka Mitatu, Na Hii Ndiyo Tarehe Atayotoa Wimbo Wake Mpya..!!

KIBA
Kwa muda mrefu wafuasi wa mwanamuziki Ally Salehe Kiba maarufu Alikiba, wamekuwa wakijiuliza sababu zilizomfanya mwimbaji huyo kukaa kando ya muziki kwa muda mrefu.
Alikiba ambaye aliachia wimbo wake wa mwisho “My Everything” Novemba 2012 hajawahi kuachia tena wimbo mwingine, licha ya kutoa kazi kadhaa alizokuwa akishirikishwa na mdogo wake msanii Abdu Kiba ukiwamo “Kidela”.
Starehe ilikaa kitako na msanii huyu aliyewahi kutamba na wimbo wake wa kwanza “Sinderela” mwaka 2007, nyumbani kwake Kunduchi Beach na ambapo aliainisha mambo makubwa matatu yaliyomfanya asimame kwa muda kuachia kazi za muziki.
“Kuna mambo matatu ya msingi niliyokuwa nayafanya kwa kipindi hiki cha miaka mitatu. Awali ya yote niliamua kusimama ili kumlea mwanangu, malezi ya mtoto yalinifanya niegemee huko hadi umri wake usogee ndipo nirudi kwenye muziki,” anasema pasipo kufafanua vizuri iwapo ni wa kike au wa kiume.
Anasema familia yake ni kitu chenye uthamani mkubwa kwake ndiyo maana alijitoa ili kuhakikisha inakaa sawa.
“Jambo la pili ambalo najivunia kulifanikisha kwa kipindi hiki, ni kuweza kumsimamisha sehemu nzuri mdogo wangu Abdu Kiba katika ramani ya muziki. Hili lilikuwa suala kubwa na nyeti kwangu kuhakikisha anatimiza ndoto zake nilijitahidi kumpa nyenzo ili na yeye ajulikane kwani nilimuona ana kipaji kikubwa,” anasema.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname