Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliohusika na utekaji na unyan'ganyi wa gari Mei 12 mwaka huu eneo la Mlima Msangamwelu Wilaya ya Mbeya Vijini wameuawa na wananchi katika mapambano makali pembezoni mwa Mlima Mbeya.
Jambazi la kwanza lilitambuliwa kwa jina la Kitwana Lugoya(30)mkazi wa Ilemi Juhudi Jijini Mbeya ambaye aliuawa na wananchi baada ya kupata taarifa ambapo walifanikwa kumzingira na kufanikiwa kumkamata eneo la Msangamwelu Kata ya Mshewe.
Juhudi za wananchi ziliendelea kwa kushirikiana na Jeshi la kuwasaka majambazi wengine ziliendelea na kufanikiwa kuwakamata majambazi wengine wawili waliotambuliwa kwa majina ya Ndayobi Lutego(26)mkazi wa Igunga mkoani Tabora na Idd Sadiki(29) mkazi wa Veta Jijini Mbeya.Hata hivyo juhudi za wananchi ziliendelea kuwasaka majambazi wengine wawili waliosalia wakiwa na bunduki na risasi kadhaa ambao walitokomea katika msitu mnene kupandisha Mlima Mbeya na kufanikiwa kukamata jambazi jingine lililokuwa na silaha na mfuko wa risasi ambapo wananchi walilidhibiti ndipo alirusha silaha na risasi msituni na kuanza kupambana na wananchi kwa kusaidiana na Askari na kufanikiwa kumkamata na katika mapambano hayo jambazi hilo liliuawa kwa kutumia silaha za jadi na mawe.
Jambazi mwingine alikamatiwa katika Kitongoji cha Lunji Kijiji cha Ihombe kwa ushirikiano na wananchi wa vijiji vya Ihombe,Iziwa,Bofya hapa Kuangalia Picha zaidi >>>>>
No comments:
Post a Comment