14 May 2014

Unaambiwa huyu ndie mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Mashariki anaetegemewa kucheza kombe la dunia mwaka huu



Mshambuliaji Divock Origi ambaye ni mtoto wa aliyekua mchezaji wa timu ya harambee stars ya Kenya Mike Okoth ametajwa kwenye ikosi cha wachezaji 24 watakaoiwakilisha Ubelgiji katika mechi za kombe la Dunia mwezi ujao nchini Brazil.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ubelgiji ya under-21 ambapo pamoja na yeye watakaokuwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na Vincent Kompany, Eden Hazard, Romelu Lukaku, Adnan Januzaj, Marouane Fellaini, Thomas Vermaelen na Moussa Dembele.

Kwa sasa Arsenal na Liverpool wanawinda kwa karibu sana saini ya Divock Origi na huenda atakua mwanaafrika mashariki wa kwanza kucheza kwenye kombe la Dunia na endapo atasajiliwa na timu ya Arsenal ama liverpool basi ataweka rekodi ya kuwa Mwafrikamashariki wa kwanza kuchezea klabu 4 bora EPL.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname