Jeshi
la nchini Nigeria limesema linajua mahali walikofichwa zaidi ya
wasichana 200 waliotekwa wakiwa shuleni lakini hawawezi kuitaja sehemu
hiyo hadharani.
Wasichana hao walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo
linadai haliwezi kuwaachia hadi watakapobadilishana wafungwa wao na
serikali ya nchi hiyo.
Kwenye kituo cha TV cha Nigeria, imetangazwa kwamba japo imefahamika
walipo Wasichana hao ambao bado wanashikiliwa mateka….. majeshi ya
Nigeria na mengine yanayoendesha opareshen hiyo hayatotumia nguvu za
kijeshi kwenye uokoaji wa wasichana hawa.
Kitendo cha kutekwa kwa wasichana hao kimeibua majonzi makubwa
miongoni mwa wazazi na kufanya kuibuka kwa kampeni iliyosambaa katika
mitandao ya kijamii na vyombo vya habari yenye jina la Bring Back Our
Girls ikimaanisha “Rudisheni wasichana wetu”
No comments:
Post a Comment