Mwimbaji Injili adaiwa kumbaka shemejiye
Mume wa mwimbaji
maarufu wa nyimbo za Injili, (jina
tunalihifadhi kwa sasa), anatuhumiwa
kumbaka shemeji yake mdogo (17).
Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa juzi
saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi
Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu
mwanamume huyo kwamba alimbaka
binti huyo mara tatu na
kumsababishia maumivu makali.
Binti huyo alifika katika kituo hicho
cha polisi akiwa na ndugu zake wawili
ambao walilalamika kwamba
kulikuwa na jitihada kubwa kutoka
upande wa mtuhumiwa wa kuzima
kesi hiyo.
Akizungumza na gazeti hili nje ya
kituo hicho, binti huyo alisema
shemejiye alimbaka mara ya kwanza,
Ijumaa iliyopita na Jumapili
alipombaka mara mbili ndani ya gari.
Alisema mara ya kwanza alikaa kimya
baada ya mtuhumiwa kumtishia
kwamba angemdhuru kama angetoa
taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa
wakiwa sebuleni nyumbani kwako
Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa
taarifa kwa ndugu zake baada ya
kubakwa mara ya pili.
Polisi katika kituo hicho walithibitisha
kupokea taarifa za tukio hilo lakini
walishindwa kwenda kumkamata
mtuhumiwa kwa maelezo kwamba
hawakuwa na askari wa kutosha na
kuahidi kwamba angekamatwa jana.
Hata hivyo, hadi jana mtuhumiwa
huyo alikuwa hajakamatwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,
Marietha Minangi kutwa nzima ya
jana hakupatikana kuzungumzia tukio
hilo na kila simu yake ilipopigwa (kati
ya saa nane mchana na saa mbili
usiku), ilipokewa na msaidizi wake
akisema bosi wake ana kazi nyingine.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
alisema hakuwa amepokea taarifa
yoyote ya aina hiyo.
Mwimbaji anena
Alipoulizwa jana, mwimbaji huyo
alisema kwa sasa hawezi
kuzungumzia kwa undani tuhuma
zinazomkabili mumewe na kwamba
alikuwa anajisikia vibaya kutokana na
tukio hilo kuhusisha watu wake wa
karibu.
“Of course (bila shaka), hili sio tukio
zuri. Kwa sasa sina uwezo wa
kuzungumza kwa sababu hili suala
lipo Polisi. I am confused
(nimechanganyikiwa), ukizingatia
kwamba linasemekana kutokea
wakati sikuwepo nyumbani, naomba
tuzungumze baada ya akili kutulia,”
alisema.
Kadhalika, jana saa 6:20 mchana,
gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na
mtuhumiwa ambaye baada ya
kupewa maelezo kuhusu tuhuma
zinazomkabili alisema: “Samahani
sana ujue sikusikii kabisa,” kisha
alikata simu.
Gazeti hili lilimpigia tena simu lakini
ilikatwa na baada ya hapo kila
alipopigiwa haikupokewa. Baadaye
saa 6:35 mchana, mtu
aliyejitambulisha kuwa ni mdogo wa
mtuhumiwa alipiga simu chumba cha
habari akitaka kuonana na mhariri wa
gazeti hili, kwa maelezo kwamba
alipewa namba husika na kaka yake.
“Samahani, mimi (anataja ina) niko
hapa nje Ofisi za Mwananchi, nilifika
hapa kutaka kuonana na mhariri
maana nasikia mwandishi wenu
alikuwepo polisi tangu jana kwenye
tatizo lililompata kaka yangu, sasa
wakati nasubiri kuonana na mhariri
kaka amenipigia simu akisema
namba hii imempigia, kwa hiyo
naomba tuonane ili tuzungumze
tuone jinsi ya kumsaidia,” alisema.
Baada ya kuonana na mwandishi wa
habari wa gazeti hili, alisema suala
hilo lilikuwa likijadiliwa katika ngazi
ya familia, hivyo wasingependa
liandikwe kwenye vyombo vya habari.
Vipimo vya hospitali
Juzi, baada ya tukio hilo kuripotiwa,
mtoto huyo alipelekwa katika
Hospitali ya Amana ambako
alifunguliwa faili la matibabu na
kupewa namba ya usajili 667.
Aliingia
chumba cha matibabu namba 21
kumuona daktari kwa ajili ya vipimo
zaidi.
Matokeo ya vipimo yalionyesha kuwa
binti huyo alikuwa amefanya ngono
kwa nguvu. Katika fomu hiyo ya
uchunguzi, daktari aliandika ‘High
vagina swab’.
Baada ya vipimo, familia ilirudi katika
Kituo cha Polisi kupeleka matokeo ya
vipimo vya daktari, hivyo kufungua
faili la kesi lililopewa namba RB TBT/
RB/319/2014 na namba TBT/
IR/1865/2014. Jana binti huyo
alikwenda tena Amana ambako
alifanyiwa vipimo vilivyobaki vya VVU
na mimba. Vipimo vya awali vya VVU
vilionyesha kuwa hakuwa ameathirika
na hakupata ujauzito.
Mtoto alipo
Habari ambazo zililifikia gazeti hili
jana jioni, zilisema mtoto aliyebakwa
alichukuliwa na familia ya Mchungaji
Josephat Gwajima.
Gazeti hili lilifanya jitihada za
kumtafuta Mchungaji Gwajima bila
mafanikio, lakini lilimpata mkewe,
Grace ambaye hakuwa tayari
kuthibitisha kuwapo au kutokuwapo
kwa mtoto huyo nyumbani kwake.
“Naomba nisiwe msemaji katika
jambo hilo, yupo msemaji mwenyewe
ambaye naamini mnamfahamu naye
ni Mchungaji Gwajima, kwa hiyo
mtafuteni, yeye atasema kama mtoto
yupo hapa au hayupo na kama yupo
sababu zake ni zipi,” alisema Grace.
Alipoombwa atoe mawasiliano ya
simu ya mchungaji huyo, Grace
alisema: “Kwa kweli kama unaweza,
kesho nenda pale Kanisani Kawe
utapewa utaratibu wa kuonana naye.”
No comments:
Post a Comment